Alhamisi, 7 Mei 2015

WEMA SEPETU NA DIAMOND THE PLATNUMZ WAMALIZA TOFAUTI ZAO KWA MASHABIKI

Mashabiki wa Wema Sepetu na Diamond Platnumz..Matusi Hayamjengi Mtu, Yanambomoa!Kwa mashabiki wa Wema Sepetu na Diamond Platnumz. Hawa wawili ni wasanii wetu wanaokubalika nchini, kila mmoja kwa namna yake na kila mmoja ana mashabiki wake. Waliwahi kuwa wapenzi lkn mambo hayakwenda kama mashabiki na wao walivyotaka wakaamua kwa amani kuachana. Lakini bado wanaheshimiana na hata familia zao zinaheshimiana. Na Wema Sepetu bado anamsapoti Diamond ni msanii wake wa kwanza nchini anayependa kazi zake.Mpaka hapo, ukishaelewa hayo huwezi kupata ujasiri wa kuwatukana kivyovyote. Hupendi hawako pamoja? Basi support yule unayempenda au kama unawapenda wote wawili endelea kuwasapoti sio kosa lako hawako pamoja! Ni kwa faida yao nzuri tu yenye nia njema. Heshimu mawazo yao...... Sijui khs nia ya team diamond...ila naomba nieleweke kwa wanaompenda Wema... ana projects nyingi zinakuja pia ana issue kubwa nchini ambayo itahusisha watu maalumu ngazi za juu serikalini vile vile si mnaona pia kuna suala la yeye kupigiwa kura?
Ni kwamba Wema anapendwa na watu wengi, lakini kitendo cha watu wanaotumia jina lake kutukana kitaleta makundi na watu kwa kukomoa watasapoti watu wengine au akiwa na issue hawatamsapoti ambapo si vibaya lkn sababu kubwa ni kwamba watu wanatukana sana.

Kuna wengine wanatumia kivuli cha Wema lkn ukweli hawampendi na kuna wanaotukana watu sana mpaka watu hudhan Wema anawatuma au team Wema wahuni lkn si kweli, Wema ana watu wengi wanaombeba wenye heshima zao....pia yeye Wema hatukani au kujibizana na watu kuweni kama yeye, msimchafulie mwenzenu.

Kwa namna hii watu wanaogopa kusema wanampenda Wema hadharani kwa kuhofia kutukanwa hii inampunguzia Wema marafiki. Ukweli ndo huo, sasa kama kweli unampenda Wema onyesha mapenzi yako kumsapoti na sio mwezi mzima unatukana halafu siku moja tu ndo unamsapoti wewe utakuwa sio mpenzi wa Wema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni