Jumanne, 12 Mei 2015

Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Diwani Athumani Msuya, kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Diwani Athumani Msuya, kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (Director of Criminal Investigation).
Kabla ya uteuzi huu CP Msuya alikuwa Kaimu Kamishna wa kamisheni ya Intelijensia ya Jinai. CP Msuya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Robert S. Manumba ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria.
Rais Kikwete pia amemteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Valentino Mlowola kuongoza Idara ya Intelijensia ya Jinai, kujaza nafasi inayoachwa na Kamishna Msuya.
Kabla ya Uteuzi huu, DCP Mlowola alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.Uteuzi huu umeanza tarehe 3 Mei, 2015

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
12 Mei, 2015

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni