Jumanne, 12 Mei 2015

TEITI yawanoa waandishi wa habari za biashara juu ya uwazi katika sekta ya madini nchini


 
41Mwenyekiti wa Mpango wa Uhamasishaji wa Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI), Jaji Mstaafu, Mark Bomani akifungua warsha ya siku moja kwa wadau na wandishi wa habari za biashara, mkutano uliofanyika Ledger Plaza Bahari Beach Hotel jijini Dar es Salaam, Mei 7, mwaka huu.
1Afisa mahusiano Mkuu wa TEITI, Catherine Mbatia akimkaribisha rasmi Mwenyekit wa TEITI, Jaji Mark Boman kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa Warsha hiyo iliyowakutanisha wandishi wa habari za biashara na wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa madini.
6
Meneja Mahusiano, Alex Modest, (kulia)akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika semina hiyo watatu kulia ni Meneja mikakati kutoka (TBDC) George Kibakaya (kushoto) Mwenyekiti TEITI,Jaji Bomani,wa pili kushoto mwandishi mchambuzi, John Bwire,(katikati) ni Halfani Halfani kutoka (Oil Gas Association Tanzania-OGAT).
2
Afisa mahusiano Mkuu wa TEITI, Catherine Mbatia akielezea juu ya TEITI, wakati wa Warsha hiyo iliyowakutanisha wandishi wa habari za biashara na wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa madini.
13
Mwenyekiti TEITI, Jaji Bomani (kushoto ) akichangia mada katika warsha hiyo, wengine ni Mwanahabari na mchambuzi John Bwire, akifuatiwa na Halfani Halfani wa OGAT, Meneja mikakati kutoka (TBDC) George Kibakaya pamoja na Godvictor kutoka kampuni ya madini ya Geita.
14
Wadau wa sekta ya madini na wanahabari wakifuatilia mada katika warsha hiyo.

4
Mwandishi Mwandamizi wa Mtandao wa Modewji blog, Andrew Chale (kushoto) akifuatiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la Business Times, Damas Makangale, pamoja na wandishi wengine waki 'note' vitu muhimu kwenye warsha hiyo.
9
Mwandishi wa habari na mchambuzi, John Bwire akitoa mada katika warsha hiyo juu ya umuhimu wa kuwajengea uwezo wajasiliamari wa ndani ili kunufaika na sekta ya madini tuliyonayo
12
Godvictor kutoka kampuni ya Madini Geita, akitoa mada juu ya uwazi wa makampuni hapa nchini hasa katika sualala ulipaji wa kodi na mifumo ya kisheria ya biashara hiyo ya sekta ya madini ambapo alibainisha kuwa baadhi ya makampuni yamekua yakitumia sheria ya Kimataifa hivyo uwepo wa baadhi ya makapuni hayo kutoweka wazi mikataba yao ni kuogopa ushindani katika soko la Kimataifa.
17
Mwanahabari mwandamizi Joseph Mwamunyange (kushoto) akiwa na wadau wa sekta ya madin, Kulia ni mtaalam wa uchambuzi wa data katika sekta ya madini kutoka taasisi ya Global Witness Rachel Owens wakati wa warsha hiyo
19  
Picha juu na chini Wanahabari wakiendelea na majukumu yao .. kwenye warsha hiyo
20 23
Mwanahabari Joseph Mwamunyange akiendesha mjadaraa juu ya uwazi katika masuala ya upatikanaji wa habari kwa uwazi hasa za sekta nyeti za madini na fedha.
24
Prof. Handley Mwafenga (TMAA) akitoa mada juu ya uwajibikaji na uwazi katika sekta ya madini katika warsha hiyo..
25 29
Mjumbe wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) George Kibakaya ali
30
Wadau wa sekta ya madini wakichangia mada katika warsha hiyo..
31
Dr. Camillius Kasalla kutoka (CSO) akitoa mada namna ya vyama vya kijamii NGOs juu ya umuhimu wake katika ufuatiliaji wa mambi ya uwazi katika sekta ya madini..
37
33
Samuel Osei Bekoe kutoka taasisi ya NRGI ya nchini Ghana akitoa mafunzo kwa wandishi wa habari (Hawapo pichani) ya namna ya kupata habari kupitia mitandao ya intaneti hasa ya takwimu na mahesabu ya masuala ya fedha na madini.
38
..mafunzo hayo
36
Samuel Osei Bekoe kutoka taasisi ya NRGI ya nchini Ghana akitoa mafunzo kwa wandishi wa habari (Hawapo pichani) ya namna ya kupata habari kupitia mitandao ya intaneti hasa ya takwimu na mahesabu ya masuala ya fedha na madini.
 
40
Mwenyekiti wa Mpango wa Uhamasishaji wa Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI), Jaji Mstaafu, Mark Bomani akiwa na vitabu vya ripoti ya nne, vikiwa katika lugha mbili ya kiswahili na kiingereza akivionesha kwa wadau na wandishi wa habari za biashara, mkutano uliofanyika Ledger Plaza Bahari Beach Hotel jijini Dar es Salaam, Mei 7, mwaka huu.



Na Andrew Chale, Modewji blog.
Mwenyekiti wa Mpango wa Uhamasishaji Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi Asilia na Mafuta (TEITI) Jaji Mark Boman amewataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi zenye lengo la kuielimisha jamii hasa pindi wanaporipoti habari za sekta ya madini hapa nchini.

Akizungumza wakati wa semina ya waandishi wa habari za biashara na uchumi ya siku moja iliyofanyika hivi karibuni Ledger Plaza Bahari Beach Hotel, jijini Dar es Salaam, Jaji Bomani alisema taarifa sahihi hasa za masuala ya uchumi zinahitajika kwani zikitolewa tofauti zinaweza kusababisha mkanganyiko kwa wananchi.

Alisema taasisi hiyo ilianzishwa kuwa lengo la kufuatilia sekta ya madini kwani hapo awali ilionekana kutowanufaisha wananchi. “Awali kuliwa na mkanganyiko wa kwamba sekta ya madini haiwanufaishi wazawa hivyo Serikali ilichukua hatua na kuunda kamati ya kushughulikia tatizo hilo kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta hiyo ya madini,”alisema.

Alisema chombo hicho kilianza kutoa ripoti za ufuatiliaji wa sekta za Serikali kwa makini na fedha zinazolipwa. Alisema Ripoti ya nne ambayo ni ya mwaka 2014 inaonyesha kwamba mapato ya Serikali yamekuwa yakiongezeka kila mwaka tofauti na ripoti ya kwanza iliyokuwa na hitilafu ya Dola milioni 30.

Alisema mafanikio ya utaratibu huo umesaidia taasisi za Serikali kuhakikisha kwamba kila fedha inayotoka au kulipwa inakuwa ya maandishi ili kuwa na taarifa sahihi.

Naye Mjumbe wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) George Kibakaya alieleza kuwa, kiasi cha gesi asilia kilichogunduliwa ni futi za ujazo tirioni 55 hivyo ni vyema kujipanga vizuri ili kuhakikisha kinakuza uchumi wa nchi.

Aidha, katika semina hiyo wandishi wa habari walipata pia fursa ya kujifunza namna ya upatikanaji wa data kwa njia ya mtandao huku wakishahuriwa kuwa pindi wanahabari watafutapo data, kuweza kuwasiliana na wataalam husika iliondoa mkanganyiko ikiwemo idara za kifedha, wataalamu wa hesabu pamoja na mifumo sahihi ya data hasa kupitia mifumo ya inteneti.

Mafunzo hayo ya kuripoti habari kwa kutumia uchambuzi wa data, yalitolewa na Samuel Osei Bekoe kutoka taasisi ya NRGI ya nchini Ghana ambaye alitoa wito kwa wandishi wa habari wa Tanzania hasa wanaotaka kuandika habari za kiuchunguzi katika uripoti wa mahesabu na data kuzingatia vyanzo vya taarifa vya kina na vyenye uhakika.

Ambapo alishahuri kuwa licha ya upatikanaji wa data hizo kuwa mgumu na wa sili kwa baadhi ya sekta, aliwataka wandishi kutumia vipengele muhimu na kwa ufupi bila kuweka mambo mengi ambayo yataweza kumchanganya msomaji.

Akitolea mfano wa taarifa za kiuchumi kwa Tanzania ama nchi zingine, ambapo endapo wataingia kwenye mitandao ya taasisi ya kifedha, Ikiwemo IMF, Benki kuu na zingine zimekuwa na uwazi hivyo wanaweza kupata huko taarifa ambazo zinaweza kuwasaidia kuripoti na kuleta changamoto katika nchi huku akisisitiza kutaja chanzo cha taarifa ama ripoti hiyo.

Pia wadau mbalimbali wakiwemo wataalamu wa madini na wandishi wa habari walitoa mada mbalimbali zilizojadiliwa kwa kina katika semina hiyo kwa mfumo wa mdaharo

RAIS KIKWETE AHITIMISHA ZIARA RASMI YA ALGERIA, AREJEA NYUMBANI

PICHA NA IKULU
kj2Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiaga wenyeji wake katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Houari Boumediene jijini Algiers Jumatatu May 11, 2015 baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo. kj3Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na Marubani na Wafanyakazi wa Shirika la ndege la Tassili la Algeria baada ya kuwsili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo May 12, 2015  baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini Algeria. kj4Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na viongozi mbalimbali katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo May 12, 2015  baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini Algeria. kj5Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Raymond Mushi alipowasili  kutoka Algeria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo May 12, 2015  baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini Algeria. kj6Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na  Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es salam Suleiman Kova,  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Raymond Mushi, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda  alipowasili  kutoka Algeria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo May 12, 2015  baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini Algeria.

Rais Kikwete aifariji familia ya Nyerere kufuatia kifo cha John Nyerere

mak1Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo leo asubuhi nyumbani kwa Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye John Nyerere kilichotokea hivi karibuni.Aliyesimama pembeni ya Rais ni mdogo wa marehemu Makongoro Nyerere. mak2Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya marehemu John Nyerere nyumbani kwao Msasani jijini Dar es Salaam leo asubuhi. mak3Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye John Nyerere kilichotokea juzi .Mwili wa Marehemu John Nyerere rubani wa zamani wa ndege za kivita nchini aliyeshiriki kikamilifu vita vya Uganda kati ya mwaka 1978 na 1979, unatarajiwa kusafirishwa leo kwenda kijijini Butiama mkoani Mara kwa maziko.(picha na Freddy Maro) mak4Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye John Nyerere kilichotokea juzi .Mwili wa Marehemu John Nyerere rubani wa zamani wa ndege za kivita nchini aliyeshiriki kikamilifu vita vya Uganda kati ya mwaka 1978 na 1979, unatarajiwa kusafirishwa leo kwenda kijijini Butiama mkoani Mara kwa maziko.(picha na Freddy Maro)

MWANAHARAKATI WA BURUNDI AOMBA MKUTANO WA KESHO WA MARAISI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUTOMRUHUSU RAIS NKURUNZIZA KUGOMBEA MUHULA WA TATU.

 Mwenyekiti wa Chama cha UPD-Zigamimbaga, ambaye pia ni mwanaharakati wa vuguvugu la maandamano nchini Burundi, Mugwengezo Chauvineau. 
 
 Mwenyekiti wa Chama cha UPD-Zigamimbaga, ambaye pia ni mwanaharakati wa vuguvugu la maandamano nchini Burundi, Mugwengezo Chauvineau (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mvutano wa kisiasa dhidi ya rais wa nchi hiyo ambapo amewataka viongozi wa nchi za Afrika Mashariki wanaokutana leo jijini Dar es Salaam kutokubaliana na maamuzi ya Rais Pierre Nkuruzinza kuwania nafasi hiyo kwa awamu ya tatu.
Hapa mwanaharakati huyo akisisitiza jambo kwa wanahabari.
 
Salha MohamedMWENYEKITI wa Chama cha UPD-Zigamimbaga, ambaye pia ni mwenyekiti wa vuguvugu la maandamano nchini Burundi, Mugwengezo Chauvineau, amewataka viongozi wa nchi za Afrika Mashariki kutokubaliana na maamuzi ya raisi Pierre Nkurunzinza kuwania kiti cha urais kwa awamu ya tatu.Hali hiyo itapelekea kuendelea kutoondoka barabarani hadi hapo rais huyo atakaposema hatawania kiti cha urais kwa awamu hiyo ya tatu.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, Mwenyekiti huyo alisema wanawataka viongozi wa nchi za afrika mashariki kumshawishi raisi huyo au kumlazimisha kuachana na maamuzi hayo ya kugombea madaraka ya urais kwa awamu ya tatu.
Pia kumtaka rais huyo kutoa silaha ambazo zimezagaa kwa wananchi hao, na kuandaliwa mazingira bora ya chaguzi na utendeke kwa hali ya kuwa wanasiasa wanakuwa huru na kuacha kuwindwa na kufungwa.
Hayo yamejiri baada ya rais huyo kutangaza nia ya kuwania kiti hicho kwa awamu ya tatu ambayo ni kinyume cha sheria ya katiba ya nchi hiyo.
“Hali hii inaleta kumbukumbu ya historia ya zamani kwani yalitokea kama haya ambapo kulipelekea machafuko, na kuuawa kwa wale wote ambao hawapo sambamba na maamuzi ya rais huyo,” alisema.
Alisema hali ya usalama nchini humo ni ndogo kwani silaha zimezagaa kwa wananchi, wanajeshi na mgambo ambapo inahatarisha hata usalama wa nchi zilizopakana na nchi ya Burundi.
“Katika kipindi cha miaka kumi, hakuna hata siku moja ambayo raisi Pierre Nkuruzinza kuandaa kikao rasmi baina yake na vyama vya kisiasa na badala yake huweka wawakilishi wake, hakuna hata ndugu zake ambao wamechangia kukataa muhula huo si halali anakuwa adui yake na wengine kufukuzwa kazi na kuwindwa hadi kuuawa,” alisema.
“Huu muhula wa tatu hauna faida na taifa letu na ndiyo maana tumenzisha vuguvugu ambapo hatutaacha hadi hapo atakapo sema ameachana na awamu hiyo ya tatu, kwani amepata ushauri kutoka sehemu mbalimbali kama muungano wa watu wa ulaya, Afrika yenyewe, nchi za jumuia ya Afrika mashariki lakini pia kwa maaskofu, hivi sasa anataka kuwa sababu na chanzo cha machafuko kwasababu raia wa burundi kwa uoga wamekimbia nchi yao,” alisema.
Aidha alimpongeza rais wa Jakaya Kikwete kukubali kuwakaribisha wananchi wa Burundi na kuwapatia hifadhi

Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Diwani Athumani Msuya, kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Diwani Athumani Msuya, kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (Director of Criminal Investigation).
Kabla ya uteuzi huu CP Msuya alikuwa Kaimu Kamishna wa kamisheni ya Intelijensia ya Jinai. CP Msuya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Robert S. Manumba ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria.
Rais Kikwete pia amemteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Valentino Mlowola kuongoza Idara ya Intelijensia ya Jinai, kujaza nafasi inayoachwa na Kamishna Msuya.
Kabla ya Uteuzi huu, DCP Mlowola alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.Uteuzi huu umeanza tarehe 3 Mei, 2015

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
12 Mei, 2015

WAKAZI WILAYA YA KAKONKO WATAKIWA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII CHF-KIGOMA

Katibu tawala wilaya ya Kakonko Bi.Zainab Mbunda akifungua Mkutano wa wadau wa Mfuko wa Taifa wa Afya ya Jamii CHF uliofanyika katika Ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma ambapo alisisitiza umuhimu wa wananchi kujiunga na Mfuko huo wa hiari ambao unawawezesha kupata huduma za matibabu kwa muda wa mwaka mzima baada ya kujiunga na kuchangia kiasi cha shilingi elfu kumi.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kakonko Bi.Jaina Msangi akizungumza namna ambavyo Halmashauri inavyosimamia Mfuko huo wa CHF na kueleza kuwa wamekuwa wakihamasisha Jamii kujiunga na Mfuko huo ili waweze kunufaika na huduma za Afya.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF Bw.Rehan Athuman akitoa maelezo mafupi kuhusu Mfuko wa Afya ya Jamii CHF na namna ambavyo ulivyoweza kuwafikia watanzania na kunufaika na huduma za Mfuko huo unaolenga kuboresha afya za wananchi hususani wenye kipato cha chini na cha kati.

Baadhi ya Wadau wa Mfuko wa Bima ya Afya waliohudhuria katika Mkutano huo wakiwemo Madiwani,Watendaji wa vijiji,Kata na Vitongoji,Viongozi wa Dini,Vyama vya Siasa,Mashirika,Asasi mbalimbali na Wazee Maarufu wa wilaya ya Kakonko(Picha zote na  KAPIPIJhabari.COM) 

Jumatatu, 11 Mei 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MAREHEMU JOHN NYERERE DAR


 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu John  Nyerere, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani, jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2015. Marehemu John 
anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani kwao Butiama
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati alipowasili  nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu John Nyerere. Marehemu John 
anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani kwao Butiama
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa  marehemu John Nyerere, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani, jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2015. 
Marehemu John anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani kwao Butiama
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati  alipowasili nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu John Nyerere.  Marehemu John anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani kwao Butiama.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo cha msiba wa marehemu John Nyerere, wakati  wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani, jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2015. Marehemu John anatarajia kuzikwa  keshokutwa nyumbani kwao Butiama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya viongozi na waombolezaji nyumbani kwa Mama Maria  Nyerere Msasani jijini Dar es Salaam, leo wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu John Nyerere. Marehemu John anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani 
kwao Butiama. Picha na OMR

RAIS KIKWETE KATIKA SIKU YA PILI YA ZIARA YAKE RASMI NCHINI ALGERIA

 
3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelaziz Bouteflika katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
5
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na waandishi wa habari baada ya  kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
7
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa ameongozana na Rais wa Baraza la Nchi ya Algeria Mhe. Abdulkhader Bensalah akiwasili katika ukumbi wa El-Mithak Residency jijini Algiers kwa dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelaziz Bouteflika katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo. 
8
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa  na Rais wa Baraza la Nchi ya Algeria Mhe. Abdulkhader Bensalah na viongozi wengine wakipata picha ya kumbukumbu na kikundi cha utamaduni  katika ukumbi wa El-Mithak Residency jijini Algiers baada ya  dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelaziz Bouteflika katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo. 
9
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akisalimiana na mabalozi wa nchi za Kiafrika katika ukumbi wa El-Mithak Residency jijini Algiers baada ya  dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelaziz Bouteflika katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Algiers Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo. 
10
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelmalik Sellal katika  kiunga cha Ikulu ya nchi hiyo cha  Zeralda Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
11
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa viongozi mbalimbali na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelmalik Sellal katika  kiunga cha Ikulu ya nchi hiyo cha  Zeralda Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
12
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Algeria Mhe. Abdelmalik Sellal katika  kiunga cha Ikulu ya nchi hiyo cha  Zeralda Jumapili May 10, 2015 katika siku ya pili ya ziara yake rasmi ya siku tatu nchini humo.
PICHA NA IKULU